New Post

Monday, July 18, 2022

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MIKOA MBALIMBALI SENSA

 TO JOIN OUR TELEGRAM GROUP CLICK HERE

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI 

 

Mwenyekiti Kamati ya Sensa Wilaya ya Kibaha anawataarifu Waombaji kazi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha walioomba kazi za Muda za Sensa kupitia tangazo la tarehe 05/05/2022, lililotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 19 Julai, 2022 hadi 20 Julai, 2022 katika maeneo yaliyoainishwa kwenye orodha ya majina ya waombaji walioteuliwa kufanya usaili. i. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:- ii. Usaili wa Mahojiano ya ana kwa ana utafanyika tarehe 19 - 20 Julai, 2022, kwenye ofisi za kata husika. Nafasi ya usimamizi wa TEHAMA utafanyika katika ukumbi wa Halmashauri Kisabi. iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi; iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Mpiga kura, Kitambulisho cha Uraia (NIDA) na leseni ya udereva. v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, Cheti cha Kuzaliwa, Cheti cha Kidato cha IV na vyeti vya taaluma au uthibitisho wa uzoefu wa kazi za takwimu. vi. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results” au hati za matokeo za kidato cha IV (form iv results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI; vii. Kila msailiwa atajigharamia nauli, chakula, usafiri na malazi viii. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU, NACTE naNECTA); ix. Kwa waombaji wa kazi ya Msimamizi wa TEHAMA wafike na Cheti cha TEHAMA x. Uthibitisho wa Uzoefu wa kazi za Kitakwimu zinazotumia Teknolojia ya Kieletroniki kwa msimamizi wa TEHAMA xi. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo.  

DOWNLOAD PDF HERE

DOWNLOAD PDF HERE

DOWNLOAD PDF HERE

DOWNLOAD PDF HERE

DOWNLOAD PDF HERE